Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandarini na
shirika la
reli Tanzania(TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji
na uingizaji mizigo bandarini. Katika maongezi ya awali meneja wa
bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini
waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya
waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.
Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.
Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la
reli na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa
haijatekelezwa.
Thursday, December 3, 2015
WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA BANDARINI LEO
MAFINGA YETU BLOG
Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
POST A COMMENT