Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015
ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431yaliyopitia kwenye bandari
hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali
ULE “moto”
aliouwasha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Kassim Majaliwa
kwenye bandari ya Dar es Salaam wiki iliyopita, na kukolezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
wa kumsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Rished Bade, umeendelea kusambaa
kwenye eneo lote la bandari na viunga vyake baada ya leo tena Bw. Majaliwa
kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta makontena mengine 2431yenye bidhaa hayajulikani
yaliko.
Baada
ya kugundua hilo tena kwa ushahidi wa nyaraka, Waziri
Mkuu ambaye wiki iliyopita aliahidi kuwa "Tunataka ku-deal na wajanja
wajanja wa TRA." ameagiza kabla ya jua kuzama leo hii Desemba 3, 2015,
awe amepata majibu
ya kina na timilifu juu ya “uhuni” huo uliofanywa na watumishi wa umma pale
bandarini. Waziri Mkuu pia alifanya ziara kama hiyo pale stesheni kuu ya reli iliyo chini ya Kampuni ya Reli Tanzania TRL
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es salaam
kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015.
0 comments:
POST A COMMENT