HAKIMU AKAMATWA NA TAKUKURU AKIPOKA RUSHWA TSHS 250,000 | MAFINGA YETU BLOG
Breaking News
Loading...

Sunday, March 20, 2016

HAKIMU AKAMATWA NA TAKUKURU AKIPOKA RUSHWA TSHS 250,000

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemkamata Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Ngarenairobi Wilaya ya Siha, Gustavu Mallya (31), akituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 250,000 ili atoe dhamana kwa mshtakiwa mmoja anayekabiliwa na kesi ya jinai.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola.
Kamanda wa Takukuru mkoani Kilimanjaro, Alex Kuhanda alithibitisha kukamatwa kwa Hakimu huyo, baada ya kuwekewa mtego na maofisa uchunguzi wa taasisi hiyo.
“Huyu Hakimu Mallya alikuwa ameomba rushwa ya Sh. 300,000 kwa mshtakiwa mmoja, ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya wizi pamoja na shambulio la kudhuru mwili," alisema Kuhanda.
"Lakini alipewa Sh. 250,000 baada ya makubaliano na ndugu wa mshtakiwa na kisha akatoa dhamana hiyo."

google+

linkedin

MAFINGA YETU BLOG
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    IDADI YA WASOMAJI