Mbuzi Na Kondoo 200 Wakatwakatwa Mapanga Wakituhumiwa Kuvamia Shamba La Mkulima Huko Mvomero Morogoro | MAFINGA YETU BLOG
Breaking News
Loading...

Tuesday, February 9, 2016

Mbuzi Na Kondoo 200 Wakatwakatwa Mapanga Wakituhumiwa Kuvamia Shamba La Mkulima Huko Mvomero Morogoro



Zaidi ya Mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero Mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la Mwanu ' 
 
Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu ekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya kimasai
 
Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.
 
Waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio .

google+

linkedin

MAFINGA YETU BLOG
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    IDADI YA WASOMAJI